Dumagrad Books
Livres Canada Books
View Rights PortalAl-Alia Publishing House produces stories for children. Not only the child enjoys the new experience of reading Alia presents, but so as everyone else.
View Rights PortalTumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine ni mkusanyo wa hadithi fupi zilizoandikwa na waandishi waliobobea na wale wanaochipuka katika uandishi wa utanzu wa hadithi fupi. Hadithi katika mkusanyo huu zimeandikwa kwa ubunifu na kwa kuzingatia maswala ibuka katika jamii inayokwenda na utandawazi na usasaleo. Mkusanyo huu unaangazia maudhui mbalimbali kama vile: siasa, dini, ulemavu, masuala ya kijinsia, elimu, ukware, ulaghai, uchumi, mazingira, umaskini, uongozi, ukabila, mapenzi, ndoa, ushirikina miongoni mwa mengine. Masuala yaliyoshughulikiwa katika mkusanyo huu yataibua ilhamu ya msomaji, msomi, mtafiti na wanafunzi katika maisha yao. Maudhui, mtindo, lugha na uhusika ni viungo vilivyosukwa kwa namna ya kipekee katika mkusanyo huu. Wahariri -,,wakusanyaji wa mkusanyo huu ni waandishi na watunzi wa kazi za fasihi wenye tajriba na uzoefu wa muda mrefu. Mafunzo ya hadithi katika mkusanyo huu yanawagusa watoto, watu wazima, vikongwe, wageni na wenyeji.